WARAKA KWA RAILA
Mheshimiwa Raila maarufu baba ,mwanzo nakupa mkono wa tahania, nakuvulia kofia baba. Wewe kweli ni mzalendo wa kindakindaki johari wa nyoyo za wazalendo na hata wahafidhina. Anayeonja asali huchonga mzinga walisema mababu, falsafa ambayo ni tofauti na inahitalifiana na jinsi mambo yalivyo kwako. Uliyeumwa na nyuki ukichonga mzinga hurini tena asali bali waliokupinga enzi hizo ndio huvuna mahindi yenye magunzi makubwa si ibura baba. Mbona moyo unadunda mdundo wa kujuta ukiniambia umehainiwa? Sina jibu mwafaka ila dhana kwa yakini yasema una jibu. Jibu kupigania haki bila kuchelea na kama si yetu basi jipiganie upate tunda la jasho lililolovya kwa mikaka sasa na ukishindwa, chozi lako la kila kuchao liwasute dawamu na nafsi ziwakashifu. Leo wanakuita mkongwe kwa tadi wanasahau kuwa ganda la muwa wa jana ni mavuno kwa mchwa, wanasahau palipo na wazee hapaharibiki neno, wakaenda kitalifa zaidi kukuita weye mganga na kughafilika kuwa gangaganga zako ndizo tumaini la Kenya na kukuweka katika ulingo wa wakombozi ukawa sawia na mkombozi wa manasara wa taifa letu. Kejeli na dhihaka sisemi madaha na madahiro wanayokufanyia wale uliowezesha uhuru wao, Hhh inauma baba. Ama kweli wanadamu wana maudhi, wakosa uelewa na ufahamu yaani wagongwa katika nafsi zao dhilifu. Umefanya mengi kuzuia sokomoko katika taifa tukufu mradi tusisongolewe sisi wanyonge, wengine wanazidi kutendea tadi ili wafuasi shakiki wazue zani ila kwa udhubuti na imani umesema ima fa ima amani idumu. Baba sina nambako ya simu waama waraka huu ni kiakisi cha ninavyohisi na wengine wengi. Uusome upate faraja nasi tufarijike.
Wako mwaminifu
Kipenzi cha Rinah
Mweledi160zuberi AMA
Comments
Post a Comment