NINAPOBANWA.

Kupapatika kwa mtima wangu kunazua maswali ainati yanayohitaji ufahamu angavu katika ulingo wa siasa. Mashaka ya wzpiga kura takriban milioni ishirini na mbili nchini yamejaa moyoni. Nimeamua kufanya fundo siku ya mashaka, fundo yangu ni kupitia uandishi uliosheheni maswali kwa wanasiasa tuliowatuma kwa tasihili lakini wametughafali na kutupuuza. Wengi wenu mmetulekeza wenzenu tuliodamka alfajiri kuenda kituoni kuwaajiri, huku umande na baridi shadidi zikishirikiana kutuadhibu. Mara ngapi tunawaamini hasa mnapokuwa wastaraabu kutuomba kilicho chetu tukijua mtatuauni lakini hatimaye yanapotimia hamtujali tena . Kila mkija hoja na maoni yetu mnapokea kwa ufasaha na usanifu wa kumithilika tusijue kuwa mnatupatia tu usikivu lakini asilani moyo usielewe. Vipi kuhusu zahanati zile tuliowaambia kuwa zina uchache wa dawa? Ni mabadiliko yepi mpaka hospitali kuu ya kaunti in vitanda vya teremka tukaze?

Sisemi kitu labda mwataka tufe halafu matabibu nao watufuate kisa kikiwa ni njaa inayowakabili na kuwakingama kuhudumia wagonjwa kwa utuvu unaohitajika. Mnatuzika katika kaburi la sahau maadamu tulikosa busara tukakubali vibaba vyenu vya unga na shilingi Mia zenu na sasa twaathirika si haba laiti tungeenga kabla kujenga.Si kuzoroteka kwa uchumi, si bei za bidhaa za kimsingi kupanda maradufu na hamjali hambali wala wengi hawana maono ya kutukwamua kiuchumi. Azimio lenu ni kurudi kutufumba macho tena, Aise! Tumekengeuka kupevuka kimawazo,tukikuita jagina basi nenda ukatupiganie.Tusioneane mashaka urafiki wetu ukaisha.

Comments

  1. Sadakta mkuu ,,ufanisi Ni Waki,,,ueledi unao,,,endelea vivyo hivyo

    ReplyDelete
  2. Uzuba tuliokuwa nao hapo awali umetutoka njama zao tumezijua hawatudanganyi tena

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

LONG PETAL OF LOVE

A LETTER TO DP DR WILLIAM RUTO